img

Ukraine yaionya NATO kuzirejesha silaha za nyuklia ili kuikabili Urusi

April 16, 2021

Ukraine imeonya kwamba inafikiria kuzipata silaha za nyuklia ili kulinda nafasi yake ya kijeshi katika vita vyake dhidi ya Urusi ikiwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO haitakubaliana na masharti yake ya kuipa uanachama wa muungano huo wa magharibi. 

Akizungumza na kituo cha radio cha Deutschlandfunk cha Ujerumani jana balozi wa Ukraine nchini humo Andriy Melnik ameibua uwezekano wa taifa hilo la uliokuwa muungano wa Kisovieti kuzipata silaha hizo ambazo iliziachia baada ya kuvunjika kwa muungano huo mwaka 1991 na kuangazia namna ya kuzifikisha nchini humo.

Ukraine iliwahi kuwa taifa la tatu ulimwenguni kwa kumiliki silaha za nyuklia lakini liliachana na silaha hizo mwaka 1994 baada ya kuhakikishiwa usalama na Marekani, Urusi na Uingereza lakini imeelezea ghadhabu yake baada ya Urusi kulinyakua eneo lake la Crimea na kusema makubaliano hayo hayatekelezwi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *