img

Tetesi za soka kimataifa

April 16, 2021

 West Ham wanaamini wataweza kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 21, mwishoni mwa msimu.

Manchester United wapo tayari kumsajili beki wa klabu ya Fiorentina na timu ya taifa ya Serbia Nikola Milenkovic, japo dau la usajili la beki huyo ni pauni milioni 38. (Sun)

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Norway Erling Braut Haaland

Miamba ya soka ya Uhispania klabu za Barcelona na Real Madrid zinaweza kuangukia pua katika mbio za usajili wa mshambuliaji hatari wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya Taifa ya Norway Erling Braut Haaland, 20. Mshambuliaji huyo anataka dau la Euro million 35 kwa mwaka, day amble Barca na Madrid hued wasilifikie. (Goal)

Paris St-Germain wanamshinikiza mshambuliaji wao tegemezi Kylian Mbappe, 22, kusaini mkataba mpya, japo Mfaransa huyo hataki mkataba huo uwe mrefu. (L’Equipe – in French)

West Ham wanaamini wataweza kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 21, mwishoni mwa msimu. (Evening Standard)

Wolves watatupa karata yao katika mbio za usajili wa mshambuliaji wa Benfica Carlos Vinicius, 26, mwishoni mwa msimu baada ya Tottenham kuamua kutompa mkataba mchezaji huyo ambaye yupo Spurs kwa mkopo. (TVI24 – in Portuguese)

Manchester United na Arsenal wanahusishwa na mpango wa kutaka kumsajili kiungo kinda wa klabu ya Rennes, Mfaransa Eduardo Camavinga, 18, amble ameamua kutoongeza mkataba na klabu yake ya sasa. (Marca)

Manchester United wanataka beki wa Denmark Joachim Andersen, 24, ambaye anaichezea Fulham kwa mkopo akitokea Lyon. (B.T – in Danish)

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amekanusha uvumi kuwa amefanya mazungumzo na klabu ya Bayern Munich ili kuchukua nafasi ya Hansi Flick. (ESPN)

Bayern wanamfikiria kocha Massimiliano Allegri kama mbadala wa Flick. Allegri hana timu toka alipoondoka Juventus mwaka 2019. (Sport Mediaset – in Italian)

Chelsea bado wangali katika mawindo ya beki wa Uruguay na Atletico Madrid Jose Maria Gimenez, 26, lakini chaguo lao la kwanza ni beki wa Sevilla Jules Kounde, 22. (La Razon – in Spanish)external-link

Barcelona watatuma ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32, amble anaondoka klabuni halo mwishoni mwa msimu, lakini Barca hawataweza kufikia dau la mshahara lilitolewa na Juventus la Euro million 10 kwa msimu kwa mshambuliaji huyo. (Sport)external-link

Spurs wanapiga darubini za kumsajili mshambuliaji raia wa Austrian Sasa Kalajdzic,23, ambaye anachezea klabu ya Stuttgart. (Eurosport)external-link

Manchester United wamehuisha nia yao ya kumsajilili kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 26. Kiungo huyo pia anafuatiliwa na Real Madrid na PSG.(Gazzetta – in Italian)external-lin

Juventus wanampango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Ousmane Dembele, 23, mkataba wake utakapoisha 2022. (Mundo Deportivo – in Spanish)external-link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *