img

Prince Philip: Wafahamu watu 30 watakaoshiriki mazishi ya Mwanamfalme Philip kesho

April 16, 2021

Dakika 4 zilizopita

Prince Philip

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kasri ya Buckinham, ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza saa tisa alasiri, sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.

Watoto wanne wa Mwanamfalme Philip na Mtawala wa Edinburgh watalisindikiza jeneza la baba yao katika shughuli ya ibada ya mazishi hapo kesho.

Wanamfalme Charles, Andrew, Edward dada yao Bintimfalme Anne, pamoja na wajukuu wa Malkia Wanamfalme William na Harry, watatembea pembezoni mwahaha gari aina ya Land Rover amble litaubeba mwili wa Mwanamfalme Philip kuelekea katika kanisa la Mtakatifu George katika kasri ya Windsor.

Idadi ya watu walioalikwa kushiriki mazishi hayo ni 30, wakiwamo ndugu watatu wa mwanamfalme Philip kutoka nchini Ujerumani.

Wageni wote watavalia barakoa na hawatakaribiana kama inavyoelekezwa kaika muongozo wa kudhibiti virusi vya corona. Malkia Elizabeth atakaa hema ya peke yake.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kasri ya Buckinham, ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza saa tisa alasiri, sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.

The Duke of Edinburgh in May 2009 with the now the Countess Mountbatten of Burma, who is one of the 30 guests

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Mkuu wa kaunti ya Mountbatten ya Burma – anayeonekana hapa na Mwanamfalme Philip mwaka 2009 – atakuwa ni miongoni mwa wageni 30 katika ibada ya mazishi

Princess Eugenie (left) and Princess Beatrice in 2016

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Wajukuu wote wa Mwanamfalme Philip- ikiwa ni pamoja na Mwanamfalme Eugenie na Beatrice – watahudhuria mazishi

Wafahamu watu 30 walioalikwa:

Watu wote 30 watakaoshiriki ni ndugu wa karibu wa Malkia Elizabeth na mumewe Mwanamfalme Philip.

Orodha hiyo ya wageni inaongozwa na Malkia mwenyewe na watoto wake wanne.

Pia watakuwepo wenza wa watoto wa Malkia, mke wa Mwanamfalme Chalres, Camilla Duchess wa Cornwall, mume wa Bintimfalme Anne Bw. Timothy Laurence na mke wa Mwanamfalme Edward Sophie Countess wa Wessex.

Unaweza pia kusoma:

Wengine ni wajukuu wa Malkia na Mwanamfalme Philip wakiongozwa na Mwanamfalme William pamoja na mkewe Kate Duchess wa Cambridge, Mwanamfalme Harry, Bintimfalme Beatrice na mumewe Edoardo Mapelli Mozzi, Bintimfalme Eugenie na mumewe

Jack Brooksbank, Peter Phillips, Zara Tindall na mumewe Mike Tindall, Lady Louise Windsor na Viscount Severn.

Wengine ni ndugu wa karibu wa familia hiyo wakiwemo watoto wa aliyekuwa mdogo wake Malkia Bintimfalme Margaret; Earl wa Snowdon, Lady Sarah Chatto na mumewe Daniel Chatto.

Ndugu wengine ni Mtawala wa Gloucester, Mtawala wa Kent, Bintimfalme Alexandra na Countess Mountbatten wa Burma.

Ndugu wa Mwanamfalme Philip kutoka Ujerumani ni; Bernhard, Mwanamfalme wa Baden, Mwanamfalme Donatus wa Hesse na Mwanamfalme Philipp WA Hohenlohe-Langenburg.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *