img

Prince Philip: Gari ambalo Philip alitengeneza muundo wake litakatumika kubeba jeneza lake Ijumaa

April 16, 2021

Dakika 6 zilizopita

The Defender was made at Land Rover's factory in Solihull in 2003

Chanzo cha picha, Reuters

Picha za Land Rover iliyobadilishwa na kuundwa na mtawala wa Edinburgh kubeba jeneza lake imetolewa.

Mtawala huyo, ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 99 wiki iliyopita, alifanya kazi kuunda gari hilo maalum kwa miaka 16, kuanzia 2003.

Marekebisho ya muundo wake ni pamoja na sehemu ya wazi ya nyuma ambapo jeneza lake litawekwa pamoja na rangi ya kijani inayotumiwa katika magari ya kijeshi

Siku ya mazishi, gari hilo la Land Rover Defender litatumika kubeba jeneza lake kwenda kanisa la St George.

Mazishi ya Prince Philip yatafanyika katika kanisa hilo katika kasri la Windsor.

Gari hilo la Land Rover ni sehemu ya mazishi ya kifalme yaliyopangwa na kasri ya Buckingham siku Alhamisi.

Watoto wanne wa mtawala huyo – Prince wa Wales, Princess Royal, Duke wa York na Earl wa Wessex – na vile vile wajukuu wake – Duke wa Cambridge na Duke wa Sussex, watafuata gari hilo katika msafara.

Mtawala wa Edinburgh alianza kuunda gari la kubeba jeneza lake kwa kushirikiana na Land Rover mnamo 2003, mwaka ambao alikuwa na umri wa miaka 82.

Prince Philip was regularly pictured driving his Land Rovers

Chanzo cha picha, TIM GRAHAM

Maelezo ya picha,

Prince Philip alikuwa akipigwa picha mara kwa mara akiendesha magari yake ya Land Rover

Philip , ambaye alihudumu katika Jeshi la Wanamaji la Kifalme katika Vita vya pili vya dunia aliomba kwamba rangi ya gari hilo ibadilishwe ili kuwa rangi ya shaba-ya kijani inayotumiwa na magari mengi ya kijeshi.

Pia aliunda sehemu ya juu ya nyuma ili kuwa wazi ambapo jeneza lake litawekwa , kwa maelezo yake halisi, pamoja na vyumba vya pembeni ili kuzuia jeneza kuteleza.

Gari pia lina vyumba vya ndani ya magurudumu vya rangi ya kijani vinavyolingana na halina nambari ya usajili .

Gari hilo la Defender liliundwa kwenye kiwanda cha Land Rover huko Solihull na Mtawala huyo alisimamia ukarabati wake kwa miaka kadhaa ikiwemo marekebisho ya mwisho mwaka wa 2019 alipokuwa na umri wa miaka 98.

Kwa kawaida gari hilo lingetumika kumsafirisha Philip kutoka Wellington Arch katikati mwa London kwenda Windsor, maili 22, lakini janga la coronavirus lilikatiza mipango hiyo ya muda mrefu.

Former US President Barack Obama and his wife Michelle have been among Prince Philip's passengers

Chanzo cha picha, WPA POOL

Maelezo ya picha,

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle ni miongoni mwa waliowahi kubebwa na Prince Philip

Philip alitumia Land Rover katika maisha yake yote ya utu uzima aliipa Land Rover Waranti yake ya Kifalme zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Prince Philip aliaga dunia katika Kasri la Windsor Ijumaa tarehe 9 Aprili. Mwili wake sasa upo katika kanisa la kibinafsi la kasri hilo.

Masharti ya kuzuia Coronavirus nchini Uingereza yanamaanisha watu 30 tu, ambao hawataruhusiwa kukaribiana ndio wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi.

Waombolezaji watakuwa wanafamilia wa Malkia na Mtawala wa Edinburgh, pamoja na jamaa zake watatu Wajerumani . Mazishi hayo yatapeperushwa kupitia runinga

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *