img

Mrundi atuzwa medali ya dhabahu kwa kutengeneza pombe bora zaidi ya mwaka

April 16, 2021

John Chris Kavakure anasema alifunzwa na nyanya yake kutengeza pombeImage caption: John Chris Kavakure anasema alifunzwa na nyanya yake kutengeza pombe

Raia wa Burundi aamejipatia medali ya dhahabu baada ya kushinda tuzo la mtu aliyetengezeza pombe bora na tamu zaidi ya mwaka.

John Chris Kavakure amejipatia ushindi huo baada ya pombe yake kwa jina Red Flo Bio kuzipiku kwa utamu pombe 3,100 zilizotengenezwa katika nchi 90 duniani.

Shindano hilo linalofahamika kama Monde selection, linaloandaliwa na kampuni ya Ubelgiji ya viwango (International Quality Institute) hushindanisha utamu wa aina mbali mbali za pombe zenye kiwango cha kileo cha 7.5.

John Chris Kavakure Mrundi ambaye pia ana uraia wa ubelgiji ameeleza kufurahishwa kwake na medali hiyo ambayo amesema inaonesha kuwa Waafrika kwa ujumla na Warundi wanaweza.

Kavakure tayari amekwisha tengeneza aina 20 za pombe katika kiwanda chake cha pombe kinachofahamika kama Les Brasseries de Flobecq kilichopo nchini, chenye uwezo wa kutengeneza lita 30,000 kwa siku.

“Bibi yangu ndiye aliyenifanya nipende kutengeneza pombe kwasababu nilikua nikiona anavyoitengeneza, anavyoweka mchanganyiko na mimi nafuata hivyo hivyo .”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *