img

Mbunge aonekana akiwa uchi wa mnyama katika mkutano wa kazini kupitia Zoom Canada

April 16, 2021

Mwanasiasa mmoja nchini Canada ameomba msamaha baada ya kujitokeza akiwa uchi wa mnyama katika simu aliyopigiwa kwa njia ya video na wanasiasa wenzake.

“Hii ilikuwa bahati mbaya,” William Amos, anayewakilisha eneo la Quebec huko Pontiac, amesema katika taarifa.

“Video yangu ilijiwasha bahati mbaya wakati ninabadilisha nguo za kazi baada ya kutoka kufanya mazoezi,” amesema.

Picha ya tukio hilo ilitumwa kwa bahati mbaya katika mtandao wa kijamii ikimuonesha Bwana Amos akiwa ameshika simu yake mkononi juu ya sehemu zake za siri. Munaweza kutoa teaser hapo.

Mbunge huyo wa liberal alionekana akiwa amesimama nyuma ya kiti karibu na dawati kati ya bendera ya Quebec na bendera ya Canada.

Twitter Bwana Amos alisema “emeaibika” na tukio hilo, ambalo analielezea kama “kosa” na kuahidi kuwa “halitawahi kutokea tena”.

“Naomba msamaha wa dhati kwa wenzangu bungeni kwa purukushani hii ambayo imetokea bahati mbaya,” alisema katika taarifa yake, alipotuma ujumbe akiomba msamaha baadaye.

Mbunge wa chama cha Bloc Québécois, Claude DeBellefeuille, amesema baada ya mkutano huo kuwa huenda “ikawa muhimu kukumbusha wabunge hasa wanaume, kwamba kuvaa tai na jaketi ni lazima “.

“Tunaona mbunge alikuwa sawa lakini nafkiri ni muhimu wakumbushwe kuwa makini na kudhibiti kamera zao,” amesema kwa Kifaransa, kulingana na shirika la habari la CTV News.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *