img

Marekani yaiwekea vikwazo Urusi kutokana na mashambulio ya kimtandao

April 16, 2021

Dakika 9 zilizopita

Vladimir Putin na Joe Biden

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Urusi ili kujibu kile inachosema ni mashambulio ya kimtandao na matendo mengine ya uadui.

Hatua hizo, ambazo zinawalenga maafisa na taasisi, zinanuia kuzuia shughuli za madhara za “Urusi katika mataifa ya kigeni “, ilisema White House.

Taarifa ilisema kuwa idara ya ujasusi ya Urusi ilikuwa nyuma ya udukuzi mkubwa uliofanyika katika “SolarWinds”, na ikaishutumu Moscow kuingilia katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Urusi inakanusha madai yote na inasema itajibu kwa ukarimu.

Vikwazo vilivyotangazwa Alhamisi vimeelezewa kwa kina katika agizo lililosainiwa na Rais Joe Biden. Vinakuja wakati kukiwa na hali tete ya uhusiana baina ya nchi hizo mbili.

Vladimir Putin - 14 April

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Bw Putin anasemekana kuwa anatathmini kuhusu kikao alichoalikwa na Bw Biden

Mwezi uliopita Marekani iliwalenga maafisa saba wa Urusi na makumi ya taasisi kuhusiana na kupewa sumu kwa mkosoaji wa serikali ya Kremlin Alexei Navalny. Urusi inasema haikuhusika.

Katika mazungumzo ya simu na rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumanne, Bw Bidenaliapa kulinda maslahi ya kitaifa ya marekani kwa “uthabiti “, huku akipendekea kufanya mkutano na Bw Putin ili kutafuta maeneo ambayo nchi mbili zinaweza kufanya kazi pamoja.

Utawala wa Biden ulisema nini?

Alhamisi, Bw Biden alielezea uamuzi wake wa kuiwekea vikwazo Urusi kama “sawia “.

“Nilikiwa muwazi kwa Rais Putin kwamba tungeweza kufika mbali, lakini niliamua kufanya hivyo ,” Bw Bidenaliwaambia waandishi wa habari. “Marekani haitafuti kuanzisha mzunguko wa kuharibu uhusiano na mzozo na Urusi.

US President Joe Biden speaks from the Treaty Room in the White House, in Washington, DC, USA, on 14 April 2021, about the withdrawal of the remainder of US troops from Afghanistan.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Joe Biden aliahidi kuchukua hatua kali kwa Urusi

Aliongeza kuwa njia kuelekea mbele iko wazi “Mazungumzo yaliyo makini na mchakato wa kiplomasia “.

Taarifa kutoka ikulu ya White House ilisema kuwa vikwazo vipya vinaonesha kuwa Marekani ” itaweka garama njia ya kimkakati na kiuchumi yenye athari ” kama itaendelea “na kitendo chake cha uyumbishaji wa kimataifa”.

Ripoti hiyo ilisisitizia tena mtazamo wa msimamo wake wa kiutawala kwamba serikali ya Urusi iko nyuma ya mashambulio ya kimtandao na imekuwa ikijaribu “kudhoofisha mwenendo wa uchaguzi wa huru na haki ” katika Marekani na mataifa washirika.

Unaweza pia kusoma:

Inalaumu hasa huduma za ujasusi wa kigeni za urusi SVR, kwa mashambulio ya kimtandao SolarWinds , ambayo yaliwapatia wahalifu wa kimtandao uwezo wa kufikia mitandao ya kompyuta ya serikali na ya kibinafsi 18,000.

Mwezi Disemba mwaka jana Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema anaamini Urusi ilikua nyuma ya mashambulio hayo.

Vikwazo vya hivi karibuni vinalenga taasisi 32 na maafisa wanaoshutumiwa kujaribu kutia ushawishi wao katika uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 “na vitendo vingine vya upotoshaji wa taarifa “.

Wanadiplomasia kumi wamefutwa kazi.

line

Urusi imejibu vipi?

Muda mfupi baada ya vikwazo kutangazwa, Wizara ya mambo ya nje ya urusi iliviita “hatua za uadui ambazo zinaibua joto la malumbano “.

“mwenendo wa aina hiyo wa uchokozi utasbabisha kisasi ,”iliongeza taarifa hiyo.

Balozi wa Marekani aliitwa katika wizara ya mambo ya nje.

Muungano wa Ulaya, Nato na Uingereza kwa pamoja wametoa tarifa zikiunga mkono hatua zilizochukuliwa na Marekani dhidi ya Urusi.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *