img

Kisa cha LaMarcus kustaafu NBA kinasikitisha

April 16, 2021

 

Nyota wa Brooklyn Nets, LaMarcus Aldridge ametangaza kustaafu kucheza mchezo wa mpira wa kikapu ligi kuu nchini Marekani NBA kutokana na maradhi ya moyo yanayomsumbua akiwa mchezoni.

LaMarcus ametangaza hivyo usiku wa kuamkia leo kupitia akaunti zake za kijamii akiandika “Huu ni muda wa kuweka afya na familia yangu mbele, Japo naendelea vizuri kwasasa lakini nilijisikia vibaya zaidi usiku ule kitu ambacho ni tishio zaidikuwahi kutokea kwenye maisha yangu”.

LaMarcus ambaye aliwahi kukipiga kwenye vilabu vya Portland Trail Blazers na San Antonio Spurs amestaafu akiwa na umri wa miaka 35 tena akiwa na wastani wa alama 19.4 na rebaundi 8.2 ambacho kimemsaidia kuzidi kujizolea mashabiki wengi tokea ajiunge na Nets mwezi uliopita.

Miongoni mwa watu waliotoa salam za pole na kutambua uwezo wa nyota huyo ni, Mkurugenzi wa NBA, Adam Silver ambaye amesema, “Afya yake ya leo  na baadaye ni muhimu zaidi kuliko mchezo wenyewe, na tunajua haukuwa uamuzi mrahisi kwake”.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *