img

Eritrea inatakiwa kuviondoa vikosi vyake Ethiopia

April 16, 2021

 

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield ameitaka Eritrea kuondoa wanajeshi wake nchini Ethiopia mara moja.

Matamshi yake yanafuatia kikao cha ndani cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na mzozo uliolikumba jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

Balozi huyo ameelezea masikitiko juu ya taarifa za ubakaji na matukio mengine yasiyosemeka ya unyanyasaji wa kingoni yanayoendelea kujitokeza kwenye eneo hilo.

Awali, Mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock aliliambia baraza hilo kwamba unyanyasaji wa kingono umekuwa ukitumika kama silaha ya vita katika jimbo hilo la Tigray, hatua iliyomsukuma balozi huyo kuhoji kuhusu umuhimu wa maisha ya watu weusi mbele ya baraza hilo.

Lowcock amesema mzozo wa kibinaadamu umezidi kuchacha katika kipindi cha mwezi uliopita, huku kukiwa na changamoto ya ufikishwaji wa misaada ya kiutu na watu wakifa kwa njaa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *