img

CCM Kibaha Mji wakerwa wanaobeza kazi za Magufuli

April 16, 2021

Na Omary Mngindo, Kibaha

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mkoa wa Pwani, kimeelezea kukerwa kwake na baadhi ya wanachama wanaotumia vibaya mitandao kuchafua kazi nzuri zilizofanywa na Hayati John Magufuli.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani Viti Maalumu Selina Wilson, mbele Mwenyekiti wa chama hicho Ramadhani Maneno, baada ya mmoja kuhoji muda wa kuondolewa picha za Hayati Rais Magufuli zilizotumika katika uchaguzi uliopita, ambapo baadhi ya maeneo bado yapo.

Mwanachama huyo kutokea Kata ya Tangini alikihoji kikao hicho ikiwa ni ziara ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa Ramadhani Maneno, ambae amlihoji ukomo wa mabango ya picha ya Hayati, akisema kuwa kwakuwa siku za maombolezo zimepita ni vyema yakaondolewa.

Baada ya kauli ya mwanachama huyo anayetokea Kata ya Tangini, ndipo Selina akaelezea kusikitishwa kwake kuhusiana kauli ya kuondolewa kwa mabango, ambapo alisema haikupaswa kutolewa na mwana-CCM.

“Nikikaa kimya ninapoona jambo linakwenda kinyume nikifanya hivyo nitakuwa nimeshiriki, mjumbe aliyemaliza kuzungumza ni mmoja wa wanachama wanaotumia mitandao kuchafua kazi nzuri iliyofanywa na Hayati Magufuli,” alisema Selina.

Aliongeza kuwa kuna group ambalo baadhi yao wanalitumia vibaya ambalo yeye amejitoa kutokanaa na kutumika visivyo, jambo linalomsikitisha huku akisema kuwa Magufuli alifanyakazi kubwa akishirikiana na Mama Samia pamoja na viongozi mbalimbali.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibaha Mji Sylvester Koka aliwaonya vijana hao, akiwataka kuacha kukejeli kazi nzuri na kubwa iliyofanywa ndani ya kipondi cha miaka motano iliyopita chini ya Serikali ya awamu ya tano, na kuendelea na hii iliyopo ikiongozwa ba rais Mama Samia.

“Vijana fanyeni kazi za kujiingizia kipato, acheni kutumia muda wenu kukosoa viongozi wa serikali, awamu hii ya miaka mitano imefanya kazi kubwa, itafika wakati utabeza na hii inayoendelezwa na rais wa sita Mama yetu Samia,” alisema Koka.

Kwa upande wake Maneno alisema kuwa leo kama wanakejeli kazi za Magufuli, kesho watageukia anazozimalizia Rais wa sita Mama Samia Suluhu, ambae alikuwa na mtangulizi wake katika kuzitekeleza.

“Niwaombe ndugu zangu hususani vijana kuweni makini na matumizi ya mitandao, binafsi siifuatilii sana kwani pamoja na kuwa na faida kubwa katika jamii, lakini baadhi yetu tunaitumia vibaya, hivyo niwaase wananchi wenzangu tuwe makoni nayo,” alisema Maneno.

Katibu wa Jumuia ya Wazazi Mussa Gama amewataka viongozi wa chama hicho katika matawi yanayotoa wanachama hao wawajadili kisha hatua zinazostahili zitumike, huku akisema chama hakiwezi kukubali kuona wanachama wanatumia mitandao kuwachafua viongozi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *