img

Biden amkaribisha White House waziri mkuu wa Japan, Suga

April 16, 2021

Rais wa Marekani Joe Biden amemkaribisha waziri mkuu wa Japan Yoshihide Suga kwenye ikulu ya White House hii leo katika mazungumzo yake ya kwanza ya ana kwa ana na kiongozi wa taifa la kigeni chaguo linaloakisi mkazo wa rais huyo wa kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na mpinzani wake China pamoja na changamoto za kiulimwengu. 

Biden na Suga pia wanatazamia kujibu ujumbe unaotolewa na rais wa China Xi Jinping kwamba Marekani na mataifa ya kidemokrasia kwa ujumla yanaporomoka kufuatia machafuko ya kisiasa na kujiondoa kimataifa kulikoshuhudiwa wakati wa utawala wa Donald Trump. 

Msemaji wa Ikulu ya White House Jen Psaki amesema jana kwamba wakuu hao pia watajadili masuala mengine ya kiusalama, ambayo ni pamoja na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *