img

Waziri wa Afya akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani kuboresha sekta ya afya

April 15, 2021

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima,Leo amekutana na kufanya mazungumzo  na Balozi wa Marekeni nchini Tanzania Mhe. Donold  Wright Kwenye ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao wameongelea vipaumbele vitatu ikiwemo kuboresha afya ya watanzania, Uwekezaji wa kibiashara pamoja na kuwawezesha vijana wa Tanzania  kiuchumi.

Katika kikao hicho kilihudhuriwa na Manaibu Waziri Dkt.Godwin Mollel, Mhe. Mwanaidi Khamis pamoja na Katibu Mkuu-Afya Prof. Abel Makubi na Kamishana wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *