img

Wazee Sababu Ya Muswada Wa Afya Kuchelewa

April 15, 2021

 

SERIKALI imesema kuchelewa kwa muswada wa Bima ya Afya kupelekwa bungeni kumetokana na kuunganisha huduma za wazee na bima hiyo.

Hayo ya yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza liloulizwa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Dk Oscar Ishengoma Kikoyo lililohoji; ” Je Serikali haioni busara kuainisha vitambulisho vinavyotolewa kwa wazee na bima ya afya ili wazee wetu wapate tiba stahiki?”.

Akijibu swali hilo Waziri Ummy alisema  “Mheshimiwa Spika, suala la kuunganisha huduma za wazee na bima ya afya ni jambo moja lililotucheleshwa kuleta muswada wa bima ya afya kwenye bunge lako,  utaratibu kama huo unafanyiwa kazi, pale ambapo serikali italeta muswada wa bima ya afya itaweka utaratibu ambao utaondoa hizi changamoto za matibabu bure kwa wazee”. alisema

Akijibu Swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Ghati Chomete aliyehoji je serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Sera ya matibabu bure kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 60 katika Halmashauri za Mkoa wa Mara inatekelezeka Waziri Ummy alisema  Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza sera ya Taifa ya mwaka 2007 na Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, kwa kufanya utambuzi wa Wazeen a kuwapatia huduma mbalimbali za Afya.

Alisema hadi Disemba 2020 jumla ya Wazee 2,344,747 wametambuliwa sawa na asimilia ya 87 ya makadrio ya Wazee wote nchini.

Kati yao Wanaume 1,092,310 na Wanawake 1,252,437. Aidha, Wazee Wasiojiweza 1,087,008 wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bure na wazee 856,052 wamepatiwa kadi za matibabu za Afya ya Jamii (CHF).

Aidha, Ummy aliwataka wabunge kutoa elimu kwa wananchi wao kuwa sio wazee wote wanapaswa kupata matibabu bure isipokuwa kwa Wazee wasiokuwa na uwezo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *