img

Wanandoa wa Banbury ‘wamnyima milionea chakula hadi kufa kuiba mali yake’

April 15, 2021

Dakika 10 zilizopita

Lynda and Wayne Rickard
Maelezo ya picha,

Lynda na Wayne Rickardwanatuhumiwa kwa kumuua mwenye nyumba tajiri

Wanandoa walimnyima chakula mwenye nyumba wao hadi kusababisha kifo chake ili waweze kurithi sehemu ya nyumba yake yenye thamani ya pauni milioni 3.5, mahakama moja imesema.

Mwili wa Anthony Sootheran ulipatikana nyumbani kwake karibu na kusini mwa Newington, Oxfordshire, Machi 2014.

Sootheran, 59, alitegemea huduma za Lynda Rickard, 62, ambaye alimuua kutimiza “tamaa yake”, mwendesha mashtaka amesema.

Hata hivyo, yeye pamoja na mume wake Wayne Rickard, 66, kutoka Oxfordshire, wamekanusha kuhusika na mauaji hayo

Bi. Rickard pia amekanusha madai ya kutekeleza mauaji kwa uzembe wake huku mume wake akikanusha madai ya kusababisha au kuruhusu kutokea kwa kifo cha mtu mzima aliyekuwa anawategemea.

Mwendesha mashitaka Oliver Saxby QC, alisema Bi. Rickard “alimnyanyasa bila huruma” Bwana Sootheran na mama yake, Joy Sootheran, aliyefariki dunia mwaka 2012.

Alisema kuwa mshitakiwa alikubali kughushi wosia wao na kutumia makumi ya maelfu ya pauni ya pesa za waliofariki dunia kama vile zao.

Anthony Sootheran

Chanzo cha picha, TVP

Maelezo ya picha,

Anthony Sootheran alifariki baada ya kuzuiliwa “kula na kunywa”, mahakama ilifahamishwa

Mwendesha mashitaka alisema nusu ya mali ya Bwana Sootheran pauni milioni 1.5 zilisimamishwa kwenda kwa Bi. Rickard baada ya watu kuhisi kuna kitu ambacho sio cha kawaida kuhusiana na wosia wao.

Alisema Bi. Rickard kisha yeye peke yake, akaamua kumnyanyasa na kumdhibiti kijana wake … kwa kumnyima chakula na maji”.

Aliendelea kusema “Akisaidiwa na mume wake, Lynda Rickard walimnyima chakula Anthony Sootheran hadi akafariki dunia, na kutimiza alichokusudia … akijihakikishia alichokimezea mate.”

Bwana Saxby alisema Bwana Sootheran alipatikana akiwa amefariki dunia na daktari aliyekuwa ameenda kumtembelea Machi 18, 2014, alikokuwa akiishi na kina Rickard ambao walikuwa wapangaji wake.

Wosia bandia ulikuwa umempa Bi. Rickard shamba lake na theluthi ya nyumba yake, mwendesha mashitaka amesema.

Denise Neal (L), Shanda Robinson, Michael Dunkley (R)
Maelezo ya picha,

(Kushoto hadi kuliaLeft to right) Denise Neal, Shanda Robinson na Michael Dunkley walikana kusaini kilaghai wosia wakedeny

Rafiki watatu wa kina Richard pia nao walishawishiwa na kuingia kwenye sakata hiyo.

Shanda Robinson, 51, Denise Neal, 41 na Michael Dunkley, 49, wote wamekanusha kutia saini wosia huo licha ya kwamba walifahamu wanachofanya ni ulaghai.

Pia kina Rickard wamekanusha dai la kufanya ulaghai kwa kutumia pesa za Bi.Sootheran kuunua gari aina ya Mitsubishi Shogun.

Mshukiwa wa sita katika kesi hiyo, June Alsford, 78, amekiri kosa la kutia saini ya uwongo wosia huo akijaribu ionekane kuwa ya kweli.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *