img

Urusi kujibu vikwazo vipya vya Marekani

April 15, 2021

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema leo kuwa ni jambo lisiloepukika kwamba nchi hiyo itajibu vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi yake na kwamba imemuita balozi wa Marekani mjini Moscow kwa mazungumzo mazito. 

Rais wa Marekani, Joe Biden leo ameiidhinisha serikali yake kuweka vikwazo kwa sekta yoyote ya uchumi wa Urusi, kuiadhibu kutokana na kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2020, shutuma ambazo Urusi imezikanusha. 

Urusi imeyatoa matamshi hayo baada ya Marekani kutangaza kuwafukuza wanadiplomasia wake 10 na kuweka vikwazo dhidi ya watu kadhaa na makampuni kwa shutuma za kuingilia uchaguzi huo pamoja na uvamizi wa kimitandao kwenye mashirika ya serikali kuu ya Mrekani. Urusi inazikanusha shutuma hizo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *