img

Tetesi za soka kimataifa

April 15, 2021

 

Kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, hajaamua kuhusu ikiwa anataka kurejea Manchester United baada ya kucheza vyema kwa mkataba wa mkopo West Ham. (Goal)

Mchezaji wa safu ya kati wa West Ham na England Declan Rice, 22, anataka kujiunga na Manchester United. (Manchester Evening News)

Mlindalango wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 29, anasema “yuko wazi kwa mapya ” na kwamba hapajawa na mazungumzo ya kurefusha mkataba wake na Gunners. (Times – subscription required)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, ni mchezaji anayelengwa zaidi na Barcelona kwa sasa.Timu hiyo ya ligi ya Uhispania ingependa kusaini mkataba nae katika msimu wa kiangazi lakini itasubiri mwaka ujao kama kutakuwa na haja ya kufanya. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Barcelona wanaamini kuwa watakamilisha mkataba wa uhamisho wa kiungo wa kati-nyuma wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20, kufikia mwisho wa mwezi Aprili. (Sport)

Juventus inataka kusaini upya mkataba na mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, ambaye yuko katika mkataba na Paris St-Germain. The Toffees wanataka euro milioni 50 (£43.5m) kwa ajili ya Kean, 21, au mkataba wa kubadilishana wachezaji unaomuhusisha kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 26, au kiungo wa kati-nyuma wa Uturiki Merih Demiral, 23. (Gazzetta – in Italian)

Chelsea wanaangalia uwezekano kubadilishana wachezaji kati ya kiungo wa safu ya kushoto-nyuma wa Juventus Brazil Alex Sandro, 30, na Muitalia Emerson Palmieri anayecheza katika safu ya nyuma-kushoto, 26. (Calciomercato – in Italian)

Winga wa Everton Mbrazili Bernard, 28, anasakwa na meneja wa klabu ya Real Betis Manuel Pellegrini. (Fichajes – in Spanish)

Aston Villa wameiambia Chelsea kuwa hawana haja na mkataba wa kudumu na kiungo wa kati wa England Ross Barkley ambaye kwa sasa ana mkataba wa deni. West Ham wana nia ya kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (TEAMtalk)

Liverpool wanaweza kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 18, msimu huu kukaba nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ambaye yuko tayari kuondoka wakati mkataba wake utakapokwisha. (Express)

Manchester United, Chelsea na Tottenham zote zinamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Torino na Italia Andrea Belotti, 27. (Tuttosport – in Italian)

Sporting Lisbon wanataka kumchukua mchezaji wa safu ya nyuma-kulia wa Uhispania Pedro Porro kwa mkataba wa kudumu ambaye yuko Manchester City na kufanya mkataba wa makubaliano ya kumnunua kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 wa euro milioni 8.5 (£7.4m).(Goal)

Newcastle wanahofia hali ya mkataba wa Jacob Murphy licha ya kuwa na nia na winga huyo wa English kutoka kwa klabu za Watford na Rangers. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 unaisha mwaka 2022. (Chronicle)

Kiungo wa zamani wa safu ya kulia-nyuma Ashley Young anataka kumalizia mchezo wake katika klabu ya Watford. Ashley mweny umri wa miaka 35-kwa sasa yuko katika Inter Milan. (Sun)

Arsenal huenda wakampatia mkataba kiungo wa kati-nyuma David Luiz, 33, huku meneja Mikel Arteta akiwa makini kumpa fursa zaidi mlinzi wa Mfaransa William Saliba, 20, katika mechi za kabla ya msimu baada ya mkataba wake katika klabu ya Nice kumalizika. (Football.London)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *