img

Swali la Mbunge Yustina wa Manyara Bungeni kuhusu Mawasiliano laleta matumaini

April 15, 2021

 Na John Walter-Manyara

Serikali imesema kuanzia mwaka huu wa fedha 2021/2022 wanatarajia kuanza kutangaza dhabuni kwa ajili ya kupelekeka mawasiliano katika maeneo yote yenye changamoto hiyo.

Tamko hilo la serikali limetolewa leo alhamisi april 15,2021 Bungeni jijini Dodoma kupitia Naibu waziri wa Mawasiliano ,Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew kufuatia swali la Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara Mheshimiwa Yustina Rahi ambaye aliuliza, Mfuko wa Mawasiliano kwa wote unaolenga kupeleka Mawasiliano maeneo yote ya nchi yetu, Je ni lini sasa mfuko  utawezesha upatikanaji wa mawasiliano katika kata na maeneo yasiyo na  mawasiliano katika mkoa wa Manyara?

 Akijibu swali hilo Mhandisi Mathew “amesema serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote, jukumu lake ni kuhakikisha kwamba wanafikisha mawasiliano kwa Watanzania wote hasa katika maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara kwa maana watoa huduma wengine hawatoweza kupeleka huduma hiyo kwa sababu wanaongozwa zaidi na mipango ya biashara (Business Plan) na sasa serikali inafanya tathmini katika maeneo yote ambayo yanachangamoto.

 “lakini nikukuhakikishie kwamba tumeshaanza kufanya tathmini katika mipakani pamoja na maeneo maalum ambayo yalikuwa na changamoto kubwa ambapo wabunge wamekuwa wakilalamika mara kwa mara na tathmini hiyo imeshakamilika” alisema Mhandisi Mathew

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *