img

Radi yauwa mwanafunzi Kagera

April 15, 2021

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kabugaro iliyoko kata Nyakato katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera amepoteza maisha baada ya kupigwa na radi akiwa shuleni, kufuatia mvua zilizonyesha asubuhi ya leo.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera, Dk. Mseleta Nyakiroto amekiri kupokea mwili wa mwanafunzi huyo wa kike na majeruhi mmoja wa kiume ambaye ni mwalimu katika shule hiyo, saa tano asubuhi.

Akizungumza akiwa hospitalini hapo majeruhi katika ajali hiyo ya radi Charles Alphonce ambaye ni mwalimu katika shule hiyo ya sekondari amesema kuwa wakati wa tukio alikuwa akitoa darasani kufundisha akiwa amefuatana na mwanafunzi huyo na kwamba ghafla aliona wingu kubwa la moto likishuka kuwafunika.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *