img

Putin achomwa dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19

April 15, 2021

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kuchomwa dozi ya pili ya chanjo ya corona (Covid-19).

Katika hotuba yake kwenye mkutano wa Jumuiya ya Kijiografia ya Urusi uliofanyika mtaondaoni, Putin alielezea matumaini yake kuwa ugonjwa huo utapungua hivi karibuni kutokana na chanjo inayotumika nchini.

Akibainisha kwamba alipewa dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kabla ya kuanza mkutano, Putin alisema,

“Nina hakika kila kitu kitakuwa sawa.”

Putin alipewa dozi ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 mnamo Machi 23. Wakati hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kuhusu aina ya chanjo ya Covid-19 aliyopewa Putin, mwendelezo wa chakato wa chanjo pia haukubainishwa  kwa waandishi wa habari.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *