img

Nape:Tusimshike mikono Rais Samia, tumuache aandike kitabu chake

April 15, 2021

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema Tanzania imepitia awamu tano na sasa iko awamu ya sita ya uongozi, katika awamu zote hizo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesimamia viongozi wake kufanyakazi nzuri, hivyo hamna haja ya kumshika mikono Rais Samia Suluhu.

Nape ametoa kauli hiyo leo Aprili 15, wakati akichangia bungeni Dodoma.

“Viongozi wote wamefanya mambo makubwa pamoja na marekebisho makubwa, amekuja Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu, pamoja na ndoto nzuri na mwendelezo na amesema hadharani tutaendeleza yale aliyoyaanzisha, Dk. John Pombe Magufuli, na mimi sidhani kama kuna mtu anataka haya mambo yaachwe, kama yajo mahali ni marekebisho madogomadogo na mama Samia ameanza vizuri.

“Kwa kule ambako anatakiwa kufanya maboresho ili mambo yaende vizuri mimi nadhani tumpe ushirikiano ili mambo yaende vizuri.

“Tumekuwa na vitabu vitano, sasa tunaandika kitabu cha sita, wito wangu kwa viongozi, wabunge wenzangu, wana-CCM na Watanzania tumsaidie mama (Rais @samia_suluhu_hassan kwa kumuunga mkono aandike kitabu cha awamu ya sita,” amesema Nape.

Aidha, @nape_nnauye amewasihi Watanzania kutokugombana badala yake kutoa ushirikiano ili Tanzania iweze kupiga hatua.

“Tusigombane bila sababu, Tanzania ni yetu sote, tumsaidie mama na yeye aandike kitabu chake, tusimshike mikono kumuandikia kitabu, tumuache aandike kitabu chake na ndugu zangu legacy…legacy (alama) haitetewi, legacy inajitetea yenyewe na hasa ile iliyofanywa na mtu kama Magufuli itajitetea, itajisimamia kwa miaka labda kama mtu anamashaka na legacy yake.

“Lakini kama hamna mashaka na legacy yake, basi itasikilizwa, itasemwa, itazungumzwa na sisi, watoto na wajukuu sababu haya aliyoyafanya watayakuta tu, hatuna sababu ya kugombana, hatuna sabu ya kutoana macho,” amesema Nape na kuongeza kuwa;

“Mimi nimekuwa kiongozi kwenye chama, nimesimamia idara ya maktaba na nyaraka, duniani kama kuna chama bora kimetunza nyaraka za mambo mengi ya kutosha CCM ni karibia namba moja kwa kila kitu, sasa Naibu Spika kwenye nyaraka zetu tumesema kujikosoa na kukosoana ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *