img

Khamenei: Ahadi ya Vienna kuhusu nyuklia Iran haifai

April 15, 2021

Kiongozi wa juu kabisa nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei ametupilia mbali ahadi ya awali katika mazungumzo ya Vienna ya kuyaokoa makubaliano ya nyuklia yanayosuasua kama ”isiyofaa kuangaliwa”, akijaribu kuyashinikiza mataifa yenye nguvu duniani baada ya shambulizi katika kinu cha Iran cha nyuklia cha Natanz. 

Matamshi hayo yametolewa siku moja baada ya rais wa nchi hiyo, Hassan Rouhani kuongeza pia shinikizo kuhusu makubaliano hayo. Khamenei amesema kuwa ahadi inayotolewa na mataifa yenye nguvu huwa ya kudhalilisha. Khamenei pia ameikosoa Marekani na kuionya kuwa muda unakwisha.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken ameuita uamuzi wa Iran kurutubisha madini ya urani kama ”tangazo lenye uchochezi” na linalotilia shaka uzito wa kusudi la Iran katika mazungumzo hayo. Wakati huo huo, nchi zenye nguvu Ulaya zimeionya Iran kutokana na vitendo vyake zilivyovielezea kuwa vya hatari.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *