img

Kamati Za Maadili Arusha Zaombwa Kufuatilia Maboresho Ya Mahakama

April 15, 2021

 

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Prof Ibrahim Juma ameomba ufuatiliaji wa karibu wa maboresho yanayofanywa na Mahakama ya Tanzania kwa wajumbe wa Kamati za Maadili za Mkoa na Wilaya zilizopo jijini Arusha ili kuielimisha jamii.

Prof Juma ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Tanzania ametoa ombi hilo alipofungua kikao kilichohusisha tume hiyo na wajumbe wa kamati hizo jijini humo.

“Mahakama imefanya maboresho mengi ambayo wananchi wengi bado hawajayafahamu hivyo mkiwa kama wadau wa karibu wa Mahakama najua mtafahamu mengi nanyi muende kuwaelimisha wananchi” amesema Prof Juma.

Katika hatua nyingine, Prof Juma ametoa wito kwa wajumbe wa kamati hizo kusoma taarifa kupitia tovuti na machapisho mbalimbali kuhusiana na muhimili huo kuhusiana na maboresho yaliyofanyika ili waende kuielimisha jamii kwa ufasaha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *