img

Jumuia ya Kimataifa yakosolewa kuingilia masuala ya Somalia

April 15, 2021

Serikali ya Somalia imesema inaunga mkono uamuzi wa kuongeza muda wa rais kusalia madarakani na imekosoa jumuia ya kimataifa kwa kutaka kudhoofisha michakato ya kidemokrasia ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje imesema imesikitishwa na taarifa kutoka kwa washirika wake wa kimataifa. Imesema ‘’wameelewa vibaya’’sheria za Somalia zilizopitishwa kutekeleza haki ya kidemokrasia ya watu kuchagua uongozi wao, na badala yake wameipa picha mbaya kuwa hayo ni mabadiliko yaliyo kinyume cha sheria’’.

“Kauli za uchochezi zilizojaa vitisho, ambazo zinadhoofisha uhuru wa kisiasa na haki za kiutawala za taasisi za kitaifa, zitatumika tu kuyapa nguvu mashirika ya kigaidi na makundi yasiyoitakia amani Somalia,” wizara hiyo ilisema.

Ilisema inasikitisha kuwa washirika wao wa kimataifa, kama mabingwa wa demokrasia, walishindwa kuunga mkono matakwa ya kidemokrasia ya watu wa Somalia, yaliyotekelezwa kupitia uamuzi wa bunge.

Bunge la Somalia siku ya Jumatau kwa pamoja lilimuongezea muda wa kukaa madarakani Rais Mohamed Abdullahi Farmajo pia bunge kusalia kwa miaka miwili zaidi.

Uamuzi huo, ambao Rais Farmajo ametia saini kuwa sheria, ulikosolewa na viongozi wa upinzani wa nchini humo na viongozi wa majimbo ya Jubbaland na Puntland, pia na baraza la seneti.

Wafadhili wa Somalia, ikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya, wamepinga hatua hiyo wakisema ni ya kuigawa Somalia na inayotishia utulivu wa nchi hiyo.

Washirika hao wamesema watatathimini upya mahusiano yao na Somalia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *