img

Amnesty International yaishutumu Eritrea kwa mauaji Ethiopia

April 15, 2021

Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limesema kuwa vikosi vya Eritrea vimewaua watu watatu na kuwajeruhi watu takribani 19 wakati wa mashambulizi dhidi ya raia nchini Ethiopia.

Mashuhuda waliliambia shirika hilo kuwa wanajeshi walikuwa wakipita katika mji wa Adwa katika jimbo la Tigray siku ya Jumatatu ambapo mara walianza kuwafyatulia ridasi watu waliokuwa karibu na kituo cha basi cha mji huo

Walisema kuwa wanajeshi wa Eritrea walikuwa wakifyatua risasi zilizokuwa zikitokea nyuma ya magari ya kijeshi.

Amnesty imetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kuhusu tukio hilo na kuchunguza vitendo vingine vya ukiukaji wa haki wakati wa mzozo wa Tigray uliodumu kwa karibu miezi sita.

Mwezi uliopita Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, alisema kuwa vikosi kutoka Eritrea vilikuwa vikipigana jimboni Tigray. Kwa miezi kadhaa nchi zote mbili zimekana kuhusika kwao kwenye vita hivyo.

Serikali ya Ethipia haijasema chochote kuhusu madai ya hayo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *