img

TCRA: Mawakala ruksa kusajili laini za simu mitaani

April 14, 2021

 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio la kampuni za simu nchini kuwatumia mawakala kusajili laini za simu mitaani.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 14, 2021 mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Jabir Bakari amesema mamlaka hiyo imeondoa zuio hilo na sasa kampuni za simu zitaendelea kuwatumia mawakala kufanya usajili.

Zuio hilo lilitolewa Februari 16, 2021  na utekelezaji wake ulitakiwa kuanza Mei mosi, 2021 ambapo usajili wa laini ulitakiwa kufanyika kwenye maduka ya kampuni husika.

“Kampuni za simu zinaweza kuendelea kuwatumia mawakala  bila kuathiri usajili sahihi wa laini kwa mfumo wa kibayometria.”

“Hili litafanyika wakati  tunaendelea kufanya tathmini upya ya namna bora inayoweza kutumiwa na watoa huduma kuwasimamia mawakala,” amesema akiwataka mawakala kutumia weledi katika utendaji wao wa kazi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *