img

Yanga yaitwa mezani kumchukua mshambuliaji wa simba

January 9, 2021

 UONGOZI wa Klabu ya Gwambia FC yenye maskani yao Mwanza umewaita mezani mabosi wa Yanga ili iwape mshambuliaji wao namba moja, Meshack Abraham mwenye mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara.

Abraham anawakimbiza watupiaji wote ndani ya Yanga ikiwa chini ya Cedrick Kaze ambapo Michael Sarpong,Yacouba Songne hawa wote wawili kila mmoja ametupia mabao manne.

Habari zimeeleza kuwa miongoni mwa washambuliaji ambao wamewekwa kwenye rada za mabosi wa Yanga kwa ukaribu ni pamoja na nyota huyo ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambaye pia anatajwa kuwindwa na Simba.

 Mkuu wa Idara ya Mashindano ndani ya Gwambina, Mohamed Almas amesema kuwa hawawezi kuzuia mchezaji ikiwa anahitajika na timu nyingine.

“Kama Yanga wanamhitaji mchezaji wetu Abraham ni jambo la kukaa mezani na kuzungumza, hakuna kinachoshindikana hata iwe Simba ama Azam mchezaji kazi yake ni kucheza,” amesema Almas.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *