img

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 09.01.2021: Aguero, Ozil, Brandt, Militao, Winks, Trippier

January 9, 2021

Dakika 5 zilizopita

Sergio Aguero

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero kwa uhamisho wa bure wakati kandarasi ya mchezaji huyo, 32 Manchester City itakapokamilika. (Mirror)

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema mlinda lango Sergio Romero, 33, na mlinzi, 30, Marcos Rojo, ambao wote ni wachezaji wa kimataifa wa Argentina wanaweza kuondoka klabu hiyo mwezi huu. (Manchester Evening News)

Ozil alijiunga na washika bunduki mwaka 2013

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil anafanya kazungumzo ya kujiunga na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia. Hata hivyo, Gunners imesema haitaki kulipa kiasi chochote kile cha mshahara wake pauni £350,000 kwa wiki ikiwa uhamisho huo utafanikiwa. (Guardian)

Gunners pia inahusishwa na kumnyatia winga wa Borussia Dortmund Julian Brandt, 24, mwezi huu, huku timu hiyo ya Bundesliga ikiwa yatari kumuuza mchezaji huyo wa Ujerumani wa kimataifa. (Bild – in German)

Eder Militao

Maelezo ya picha,

Eder Militao alijiunga na Real Madrid kutoka Porto mwaka 2019

Tottenham ina nia ya kumsajili mchezaji wa Real Madrid na mlinzi wa Brazil Eder Militao, 22. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Beki wa kati wa Spurs raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 31, anawindwa na PSV Eindhoven. (De Telegraaf – in Dutch)

Valencia imefanya mazungumzo na Tottenham juu ya uwezekano wakumchukua kiungo wa kati wa England Harry Winks lakini inakataa kukubali kitita kichachoitishwa na Spurs cha mchezaji huyo, 24. (AS – in Spanish)

Kieran Trippier

Maelezo ya picha,

Kieran Trippier aliruhusu Shirikisho la Soka kuchunguza simu yake ya mkononi

Mlinzi wa Atletico Madrid Kieran Trippier, 30, alikuwa anafuatilia kwa karibu uwezekano wa uhamisho Manchester United mwezi huu wa Januari, lakini uwezekano wa ndoto hiyo kutimia umedidimizwa na marufuku ya wiki 10 aliyowekewa beki huyo wa kulia wa England kwa kukiuka kanuni za mchezo wa bahati na sibu. (Talksport)

West Ham imemtambua mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 21, kama chaguo jingine katika kuimarisha kikosi chake cha kushambulia baada ya mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Sebastien Haller kujiunga timu ya Uholanzi, Ajax. Mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Joshua King, 28, Stade Reims, 24, na mshambuliaji wa Senegal Boulaye Dia pia nao wanafuatiliwa. (London Evening Standard)

Everton haifanyi mazungumzo yoyote na klabu ya Italia Roma kuhusu kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Bernard, 28, amesema kocha wa Toffees Carlo Ancelotti. (Liverpool Echo)

Juventus wanataka kumsajili tena Moise Kean

Maelezo ya picha,

Juventus wanataka kumsajili tena Moise Kean

Hata hivyo, Ancelotti yuko tayari kumuuza mshambuliaji wa Italia Moise Kean kwa Paris St-Germain ikiwa mabingwa hao wa Ufaransa wanataka kubalisha makubaliano ya mchezaji huyo ya mkopo kuwa ya kudumu. (Guardian)

Beki wa kushoto wa Manchester United Brandon Williams angependa kuhama kwa makubaliano ya mkopo katika klabu nyingine ya Ligi ya Premier, huku Newcastle United na Southampton zikihusishwa na mchezaji huyo, 20. (Manchester Evening News)

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *