img

TAKUKURU mkoa wa Mara imekamata dawa za Milioni 56

January 9, 2021

TAKUKURU mkoa wa Mara imekamata jumla ya maboksi 40 ya dawa za binadamu zilizokwisha muda wake wa matumizi, katika hopitali za serikali na vituo vya afya binafsi mkoani humo, huku wakiwashikilia watu wawili kwa tuhuma za ugawaji wa dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Alex Kuhanda, amesema kuwa dawa hizo zilizomaliza muda wake zina thamani ya milioni 56.

“Kitu ambacho hatuna uhakika nacho kama hawa wanaogawa haya madawa, wanawagawia na ndugu zao au hawawagawii lakini ni madawa ambayo yameisha muda wake, na tumewakamata watu wawili na wako ne kwa dhamana”, amesema Kuhanda.

Katika hatua nyingine Kuhanda amesema wameanza kutoa huduma ya kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kupata malalamiko na taarifa za rushwa

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *