img

Ndege ya shirika la Sriwijaya Air nchini Indonesia imepoteza mawasiliano baada ya kupaaa

January 9, 2021

Dakika 8 zilizopita

Habari za hivi punde

Ndege yenye abiria zaidi ya 50 imepoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Indonesia huko Jakarta.

Ndege hiyo ya kampuni ya Sriwijaya Air aina ya Boeing 737 imepoteza mawasiliano ilipokuwa inaelekea Pontianak magharibi mwa eneo la Kalimantan, maafisa wamesema.

Mtandao unaofuatilia safari za ndege Flightradar24.com umesema ndege hiyo imepoteza mawasiliano baada ya kupaa mita 3,000 ndani ya dakika moja.

Picha za kile kinachoonesha kama vifusi vinaonekana kwenye televisheni na mitandao ya kijamii.

Picha za kile kinachoonesha kama vifusi vinaonekana kwenye televisheni na mitandao ya kijamii.

Wizara ya usafirishaji imesema shughuli za utafutaji na uokozi wa ndege hiyo zinaendelea.

Relatives of passengers on board missing Sriwijaya Air flight SJY182 wait for news at the Supadio airport in Pontianak on Indonesia's Borneo island on January 9, 2021, after contact with the aircraft was lost shortly after take-off from Jakarta.

Maelezo ya picha,

Jamaa za waliobebwa na ndege hiyo wakisubiri taarifa rasmi za walipo wapendwa wao

Wizara hiyo imesema mawasiliano ya mwisho na ndege hiyo yalifanyika 14:40 saa za eneo.

Kulingana na taarifa za usajili, ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imetumika kwa miaka 27.

Archive photo of Sriwijaya Air plane on runway in Jakarta

Maelezo ya picha,

Picha ya ndege ya Sriwijaya Air ikipaa katika uwanja wa ndege wa Jakarta iliyochukuliwa mwaka 2009

Shirika la ndege la Sriwijaya Air, limesema bado linakusanya taarifa kuhusu ndege hiyo.

Ndege hiyo sio aina ya 737 Max aina ya ndege ambayo ilihusika katika ajali mbili mbaya miaka ya hivi karibuni.

Moja ya ajali hizo ilitokea Oktoba 2018, ikiwa ni ndege ya shirika la Indonesia Lion Air ambayo ilitumbukia baharini dakika 12 baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta na kusababisha vifo vya watu 189.

Map

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *