img

Mbunge Mlimba amaliza changamoto ya Daraja la Mto Mfuji Asaidia upatikanaji wa Sh Milioni 53 za ujenzi

January 9, 2021

MBUNGE wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godwin Kunambi amefanya ziara ya kikazi jimboni kwake amapo amefanikisha upatikanaji wa ujenzi wa Daraja la Mto Mfuji katika kata ya Masagati ambao utagharimu Sh Milioni 53 na unatarajiwa kuanza Januari 13 mwaka huu huku pia akichangia Sh Milioni Saba kwenye Afya na Elimu.

Akizungumza katika ziara yake ya kuwatembelea wananchi hao Kunambi amesema yeye aliomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Mlimba hivyo ni jukumu lake kuhakikisha wanakua na miundombinu bora ya barabara, elimu na afya.

Kuhusu Maji Kunambi amesema tayari ameshapata kiasi cha Sh Milioni 50 ambacho muda wowote kitaingizwa kwenye akaunti ili kikatumike kuleta maji tiririka lakini pia kuchimba visima kwenye maeneo ambayo maji tiririka hayawezi kufika.

” Sitaki kuwa Mbunge wa kufanya mikutano, najua kero yenu ni hili Daraja hivyo fedha hizi tulizopata zitasaidia kuanza kwa ujenzi huu, lakini pia siyo kwenye ujenzi wa barabara pekee bali ninachangia maendeleo ya ujenzi wa sekta ya Afya na Elimu, kama ambavyo wananchi wengine wanachangishwa na mimi pia nitachangia, lengo ni kufanya Mlimba yetu ipae.

Nimshukuru sana Rais Dk John Magufuli kupitia yeye tumeona namna amna ambavyo watendaji wake wa kiserikali wametusaidia kupata fedha hizi za kimaendeleo katika jimbo letu jambo ambalo litaharakisha maendeleo kwa haraka,” Amesema Kunambi.

Wananchi wa Kata hizo alizotembelea wamemshukuru kwa namna ambavyo ameonesha moyo wa upendo wa kuwakumbuka na kutimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni jambo ambapo wamesema amekua mbunge wa kwanza wa jimbo hilo kuanza kuishi ahadi zake ndani ya muda mfupi tokea achaguliwe.

Ziara hiyo ya Mbunge Kunambi imehusisha watendaji mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba akiwemo Mchumi, Katibu wa Afya, Afisa Elimu na Meneja wa TARURA ambao wamemuahidi Mbunge huyo ushirikiano mkubwa katika kuwatumikia wananchi wa Mlimba.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *