img

Democrats kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Trump

January 9, 2021

 

Wabunge wa Democrats wanapanga kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Donald Trump kwa mchango wake katika vurugu za uvamizi wa bunge zilizotokea Jumatano katika bunge la Marekani.

Msemaji wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema atawasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Bwana Trump ikiwa hatajiuzulu mara moja.

Jumatatu Democrats katika Bunge la Wawakilishi wanapanga kuwasilisha hoja kwasababu ya “kuchochea vurugu”.

Wanamshutumu Bwana Trump kwa kuhamasisha kutokea kwa fujo bungeni ambako kulisababisha vifo vya watu watano.

Rais mteule Joe Biden alisema kura ya kutokuwa na imani ni maamuzi ya bunge, lakini akaongeza kuwa “kwa kipindi kirefu tu alifikiria kuwa Rais Trump hakustahili katika kazi hii”.

Hata hivyo Ikulu ya Marekani imetupilia mbali suala la hoja ya kutokuwa na imani na Trump ikisema kwamba “inachochewa kisiasa” hatua ambayo “itasababisha mgawanyiko zaidi katika nchi hiyo bora”.

Karibu wabunge 160 wa Democrats katika bunge la Wawakilishi wametia saini hoja ambayo wabunge Ted Lieu wa California na David Cicilline wa Rhode Island walianza kuiandika wakiwa kamejificha wakati wa ghasia zilizotokea bungeni Jumatano.

Ikiwa mchakato huo utafanikiwa, hiyo itakuwa mara ya pili kwa Bunge la Wawakilishi kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Rais Trump.

Desemba mwaka 2019, bunge hilo lilipiga kura ya kutokuwa na imani na Trump kwa makosa ya utumiaji mbaya wa mamlaka na kukataa kutoa ushirikiano kwa bunge.

Lakini bunge la Seneti lilimuondolea mashitaka yote mawili Februari 2020.

Hakuna rais yeyote wa Marekani ambaye amewahi kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye mara mbili.

Hata hivyo, matarajio ya kupitishwa kwa kura hiyo bado ni finyu kwasababu Bwana Trump ana wabunge wengi wanaomuunga mkono katika bunge la Seneti.

Na hiyo ina maanisha kuwa kupigiwa kura hiyo katika Bunge la Wawakilishi kunaweza tu kuwa hatua iliyochukuliwa kuashiria kwamba Bwana Trump anastahili kuwajibishwa kwa uvamizi wa bunge.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *