img

China yasimamisha usafiri wa umma, Hebei kutokana na corona

January 9, 2021

 

Mamlaka ya China imesimamisha usafiri wa umma katika mji mkuu wa Shijiazhaung mkoani Hebei leo Jumamosi katika jaribio la kudhibiti maambukizi mpya ya virusi vya Corona. Huduma na shughuli za kawaida zilisimamishwa kwenye barabara kuu ya jiji, 

kisha ikapanua marufuku ya usafiri wote wa umma, pamoja na teksi. Tume ya Afya ya Kitaifa hapo jana imeripoti visa 33 vipya vya maambukizi ya Covid-19 katika eneo la China Bara , kutoka idadi ya watu 53 iliyoripotiwa kabla ya kuweka sheria mpya. 

Mamlaka za China iilisema katika taarifa yake kwamba watu 14 kati ya 17 walioambukizwa walitokea Hebei, na sasa wametangaza marufuku ya watu kuondoka Shijiazhaung ambao ni mji mkuu wa Hebei na wataanzisha upimaji wa watu milioni 11 katika eneo hilo. Maafisa wa manispaa wamewamuru wakaazi wa eneo hilo kukaa nyumbani kwa angalau siku saba hata baada ya kumaliza vipimo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *