img

Akaunti ya Twitter ya Trump yafungwa kabisa

January 9, 2021

Dakika 4 zilizopita

A still image taken from video provided on social media on January 8, 2021. Donald Trump via Twitter. US President Donald Trump gives an address, a day after his supporters stormed the US Capitol in Washington,

Maelezo ya picha,

Donald Trump ameandika tena ujumbe kwenye mtandao wa Twitter licha ya kwamba akaunti yake ilikuwa imefungwa kwa muda

Rais wa Marekani Donald Trump amefungiwa kabisa akaunti yake ya Twitter kwasababu ya hatari ya kuchochea vurugu zaidi”, kampuni hiyo imesema.

Kampuni ya Twitter imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kufuatiliwa kwa karibu kwa ujumbe wa Twitter wa akaunti ya @realDonaldTrump account”.

Baadhi ya wabunge na watu mashuhuri wamekuwa wakitoa wito kwa miaka mingi mtandao wa Twitter umpige marufuku Bwana Trump.

Aliyekuwa mke wa rais Michelle Obama aliandika ujumbe kwenye Twitter Alhamisi akisema kituo cha ubunifu wa teknolojia duniani Silicon Valley kinastahili kuzuia uendelezaji wa tabia mbaya za Bwana Trump na kumfuta kabisa kama mtumiaji wa huduma hizo.

Kwanini Trump alipigwa marufuku?

Bwana Trump alifungiwa akaunti yake ya Twitter kwa saa 12 Jumatano baada ya kutoa wito kwa wafuasi wake kuvamia bunge ambao aliwaita “wazalendo”.

Mamia ya wafuasi wake walivamia bunge wakijaribu kuvuruga kikao cha kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden kama rais. Vurugu hizo zilisabbaisha vifo vya raia wanne na afisa mmoja wa polisi.

Mtandao wa Twitter baadaye ukaonya kuwa unaweza kumpiga marufuku Bwana Trump kuutumia kabisa ikiwa atakiuka tena kanuni za jukwaa hilo la mawasiliano.

Baada ya akaunti yake ya Twitter kuwezeshwa tena, Bwana Trump alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Ijumaa kuwa kampuni hiyo ilikuwa na mwisho kuchochea.

Katika moja ya ujumbe wake aliandika: “Wamarekani 75,000,000 Wazalendo walionipigia kura, Marekani Kwanza na Fanya Marekani kuwa Bora Tena, watakuwa na sauti inayosikiza siku zijazo. Hawatakosewa heshima au kuchukuliwa kwa uonevu kwa namna yoyote ile !!!”

Mtandao wa Twitter umesema ujumbe huo “unatafsiriwa kama ishara zaidi ya kuwa Rais Trump hana mpango wa kuhakikisha kunafanyika ‘mabadilishano ya mamlaka kwa njia ya amani’”.

Katika ujumbe mwingine rais aliandika: “Kwa wote ambao wameuliza, sitahudhuria hafla ya kuapishwa Januari 20.”

Mtandao wa Twitter umesema kuwa ujumbe huo “umechukuliwa na wafuasi wake kadhaa kama dhibitisho la kwamba uchaguzi huo haukuwa halali”.

Mtandao wa Twitter umesema ujumbe wote huo alioandika “unakiuka sera na kanuni katika uhamasishaji wa vurugu”.

Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

Uchaguzi wa Marekani 2020: Tazama jinsi waandamanaji walivyovamia bunge Marekani

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *