img

Akaunti ya Twitter ya Trump yafungwa kabisa

January 9, 2021

Donald Trump ameandika tena ujumbe kwenye mtandao wa Twitter licha ya kwamba akaunti yake ilikuwa imefungwa kwa muda

Rais wa Marekani Donald Trump amefungiwa kabisa akaunti yake ya Twitter kwasababu ya hatari ya kuchochea vurugu zaidi”, kampuni hiyo imesema.

Kampuni ya Twitter imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kufuatiliwa kwa karibu kwa ujumbe wa Twitter wa akaunti ya DonaldTrump account”.

Baadhi ya wabunge na watu mashuhuri wamekuwa wakitoa wito kwa miaka mingi mtandao wa Twitter umpige marufuku Bwana Trump.

Aliyekuwa mke wa rais Michelle Obama aliandika ujumbe kwenye Twitter Alhamisi akisema kituo cha ubunifu wa teknolojia duniani Silicon Valley kinastahili kuzuia uendelezaji wa tabia mbaya za Bwana Trump na kumfuta kabisa kama mtumiaji wa huduma hizo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *