img

Waliokamatwa na vipande vya meno ya tembo wahukumiwa

January 8, 2021

Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ismail Ngaile katika shauri la Uhujumu Uchumi Na. 113/2019 Januari 06, 2021 imewatia hatiani na kuwahukumu washtakiwa watatu Maro Mwita Gineraga maarufu kama Dume la Nyani, Kisuti Manzi Kanzaga na Nchama Nchama Kimore kifungo cha miaka thelathini kila mmoja (30) kwa kosa la kupatikana na Nyara za Serikali ambazo ni vipande viwili vya meno ya Tembo vyenye uzito wa Kilogramu 7.15 vyenye thamani ya shilingi Milioni 34,125,000/=.

Washtakiwa hao walikutwa na nyara hizo katika Kijiji cha Gusuhi wilayani Serengeti mkoa wa Mara. Kesi hiyo imeendeshwa na Waendesha Mashtaka Chuwa Meikasi na Nko Matatala.

Aidha, katika shauri la Uhujumu Uchumi Na.120/2019 mbele ya Ngaile Mshtakiwa Masunga Kisura ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa makosa ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na kutumikia kifungo cha miaka Ishirini(20) kila mmoja kwa makosa ya kukutwa na silaha ndani ya hifadhi na kukutwa na nyara za Serikali ambavyo ni vipande kumi vya Swala na kipande kimoja cha nyama ya Ngiri.

Kesi hiyo pia iliendeshwa na Waendesha Mashtaka wa Serikali Nko Matatala na Meikasi Chuwa

Vile vile katika shauri Na. 107/2020 mbele ya Hakimu Ngaile Mshtakiwa Mhono Nyanguge maarufu kama Buchi ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka kumi na tano gerezani (15) kwa kosa la wizi wa mifugo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *