img

Wadau waNetiboli wamlilia mwenyekiti mstaafu wa chaneta Anna Bayi.

January 8, 2021

John Walter-Manyara

Wadau wa mchezo wa Netiboli nchini wameeleza kusikitishwa na kifo cha aliyekua mwenyekiti mstaafu wa chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA)  Anna Bayi na kuwa wataendelea kuuenzi mchango wake katika kukuza mchezo huo.

Wakizungumza na Kituo hiki wadau wa mchezo huo wamesema kuwa kifo chake ni pigo kubwa katika tasnia ya mchezo wa Netiboli.

Mkuu wa mkoa wa manyara Joseph Mkirikiti amesema kuwa marehemu Anna Bayi atakumbukwa kwa kuwa alikua  mdau muhimu wa mchezo wa Netiboli hapa nchini.

Akieleza alivyomfahamu Anna Bayi, Naibu katibu mkuu wa  Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Hilda Mwakatobe amesema wamepata pigo kwa kumpoteza kiongozi huyo ambaye alikuwa ni kiongozi wa michezo aliyeibua vipaji vya wachezaji.

Mwakatobe ameiombea familia ya mzee Bayi katika kipindi hiki hiki kigumu walichonacho, Mungu awape nguvu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *