img

Ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kufuatia kifo cha mke mchezaji wa Yanga

January 8, 2021

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mke wa mchezaji wa Young Africans SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Bakari Mwamnyeto kilichotokea leo Januari 8, 2021.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Steve Mnguto ametuma salamu za rambirambi kwa nyota huyo akisema TPLB inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huo mkubwa.

“Ni pigo kubwa kwa kijana wetu Bakari Mwamnyeto hivyo kama familia ya mpira wa miguu ni wajibu wetu kumfariji yeye pamoja na wafiwa wengine huku tukimuomba Mungu amweke mahali pema peponi marehemu wetu, Amin.” Alisema Mnguto.

Idara ya Habari na Mawasiliano

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania

Januari 8, 2020

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *