img

Trump arudi katika Twitter

January 8, 2021

Rais wa Marekani Donald Trump ameruhusiwa kutuma ujumbe katika mtandao wa twitter baada ya kufungiwa katika akaunti yake kwa saa 12.

Akichapisha ujumbe wenye maudhui ya maridhiano, alijizuia kuchapisha madai ya uwongo kuhusu wizi wa kura.

Twitter ilisema kwamba itampiga marufuku kabisa rais Trump iwapo atakiuka sheria za mtandao huo wa kijamii kwa mara nyengine.

Hatua hiyo ya twitter inaweka wazi msimamo wake ikilinganishwa na facebook ambayo ilimpiga marufuku kwa muda mara moja siku ya Alhamisi.

Twitter badala yake imempatia rais huyo onyo la mwisho.

Mapema siku ya Alhamisi mtandao wa michezo wa twitch pia uliweka marufu katika akaunti ya Trumpambayo amekuwa akiitumia katika mikutano yake ya hadhara.

Donald Trump aliandika ujumbe kadhaa Jumatano kwenye mtandao wa Twitter, na kuwaita waliovamia jengo la bunge la Capitol Hill “Wazalendo”. Pia alisema “Tunawapenda.”

Msemaji wa mtandao wa Twitter amesema: “Baada ya kuondolewa kwa ujumbe huo na kumalizika kwa zuio la kutumia mtandao huo kwa saa 12 ambalo alikuwa amewekewa, akaunti ya @realDonaldTrump imerejeshwa tena.

“Ukiukaji wowote wa sheria na kanuni za mtandao wa Twitter siku zijazo ikiwemo uadilifu au sera za vitisho vya vurugu, basi akaunti ya @realDonaldTrump itafungwa kabisa.”

Awali hapo jana, rais alifungiwa kutumia akaunti ya Facebook na Instagram. Hatua hiyo itapitiwa tena baada ya Joe Biden kuapishwa rasmi kama rais wa Marekani Januari 20.

Mtandao huo wa kijamii awali ulikuwa umeweka marufuku ya saa 24 baada ya bunge la Marekani kushambuliwa.

Mkuu wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg, aliandika kuwa hatari ya kumruhusu Bwana Trump kuweka ujumbe mtandaoni “ni kubwa mno”.

Bwana Zuckerberg alisema Facebook iliondoa ujumbe wa rais “kwasababu tulihitimisha kwamba utakuwa na athari – na kuna uwezekano mkubwa nia ikawa kusababisha vurugu zaidi”.

BBC haihusiki na maudhuiya mitandao hii ya kijamii

Alisema ni wazi kuwa Bwana Trump alidhamiria kushusha hadhi ya mabadilishano ya madaraka na rais mteule Joe Biden.

“Kwahiyo, tunaongeza zuio la kutumia mtandao wa Facebook na Instagram kwa angalau wiki mbili zijazo hadi shughuli ya ubadilishanaji wa mamlaka kwa njia ya amani itakapokamilika,” aliandika.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *