img

Tetesi za soka kimataifa

January 8, 2021

 

Manchester City inakaribia kumsaini ‘Messi mdogo’ Dario Sarmiento. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 winga wa Argentina anaichezea klabu ya Estudiantes katika ligi ya nchi hiyo.. (Talksport)

Menega wa klabu ya Fernabahce Erol Bulut amesema kwamba hali kuhusu uwezekano wa klabu hiyo kumsaini kiungo mchezeshaji wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil 32 itakuwa wazi katika siku chache zijazo “. (Mirror)

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce anataka Newcastle kuwasaini wachezaji watatu wa England wanaochezea Man United kwa mkopo mwezi huu na amezungumza kwa muda mrefu na klabu yake ya zamani kuhusu winga Brandon Williams, 20, beki Phil Jones, 28, na kiungo wa kati Jesse Lingard, 28. (90min)

Newcastle pia imewasilisna na Monaco kuhusu beki wa Ufaransa Djibril Sidibe, 28. (Foot Mercato – in French)

Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche ametaka chanjo ya corona kuharakishwa katika soka huku fedha zinazohifadhiwa kuwapima wachezaji zikiepelekwa katika idara ya afya.. (Guardian)

Kiungo wa kati wa Man United na Uholanzi Donny van de Beek huenda akaondoka kulingana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Dimitar Berbatov. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameanzishwa katika mechi mbili za ligi msimu huu baada ya kusainiwa kwa dau la £35m mwezi Septemba. (Betfair via Sun)

Kipa wa Man Unted na Argentina Sergio Romero, 33, anatarajiwa kurudi katika klabu hiyo wiki ijayo huku mazungumzo kuhusu hatma yake yakiendelea. (Sky Sports)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich amepeana baadhi ya vyumba vya hoteli ya Stamford Bridge kwa wafanyakazi wa Afya NHS kwa mara nyengine (Independent)

Mkufunzi wa Watford Xisco Munoz ameambia wachezaji wake ‘kucheza kama wanyama’ wakati wa mechi ya FA dhidi ya Manchester United (Evening Standard)

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *