img

Msaada wa magari ya kijeshi kwa vikosi vya Peshmerge

January 8, 2021

 

Marekani imetoa msaada wa magari ya kijeshi kwa vikosi vya Peshmerge ambalo ni eneo la Utawala wa Kanda ya Kikurdi ya Iraq (IKBY) katika kipindi cha mwaka mpya.

Marekani ilitoa magari hayo mapya ya kijeshi kwa Wizara ya Peshmerge katika hafla maalum ya kukabidhiana iliyofanyika Erbil kama mwendelezo wa misaada ya hapo awali.

Wakati hakuna taarifa yoyote iliyotolewa juu ya idadi ya magari, inaarifiwa kwamba magari kadhaa kama vile aina ya Humvee yenye silaha na magari ya kubebea wagonjwa yalionekana kuwa miongoni mwa magari yaliyokuwepo kwenye hafla.

Kwa upande mwingine, ifahamike kwamba msaada huo ulikuja baada ya Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kazimi kusema kuwa nusu ya wanajeshi wa Marekani nchini humo wataondolewa Iraq katika siku zijazo.

Kazimi alitoa ujumbe kwa njia ya video hapo jana kwenye hafla ya “Siku ya Jeshi la Iraq” na kusema,

“Wanajeshi kadhaa waliondoka katika miezi iliyopita kufuatia mazungumzo ya kimkakati yaliyofanywa na Marekani, na nusu ya vikosi hivyo pia vitaondolewa katika siku zijazo.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *