img

Mipira ya kondomu yenye hitilafu yazua hisia kali Zambia

January 8, 2021

Mbunge mmoja wa Zambia amelinganisha usambazi wa mipira ya kondomu nchini humo na glavu kutokana na bidhaa hizo mbili kushindwa kuafikia viwango vya usalama na ‘mauaji ya kimbari’.

‘’Kile ambacho wizara ya afya inakifanya ni mauaji ya kimbari” mbunge Mwansa Mbulakulima aliambia BBC.

Unapoweka maji katika glavu hizo na mipira ya kondomu zinavuja. Ni watu wangapi wamefariki kuanzia mwezi Septemba kutokana na uzembe huu’’.

Mbunge huyo alisema kwamba ana wasiwasi kuhusu usambazaji wa magonjwa ya zinaana virusi vya corona.

Bwana Mbulakulima na wenzake katika kamati ya bunge walisikia siku ya Jumatano jinsi kampuni ya Honey Bee , ilipata kandarasi ya kusambaza mipira ya kondomuna glavu ambazo zilikua na hitilafu.

‘’Glavu hizo zinapaswa kutumika na wafanyakazi wa afyawanaokabiliana dhidi ya virusi vya corona na zimesambazwa kote nchini licha ya kuwa na hitilifu’’, alisema bwana Mbulakulima.

Mkurugenzi wa Imran Lunat aliishutumu afisi ya mkaguzi mkuu kwa kuwa na upendeleo katika ripoti yake iliobaini kwamba kampuni hiyo haina ofisi ya moja kwa moja kulingana na ripoti ya gazeti la serikali Daily Mail.

Ukaguzi huo pia ulibaini kwamba kandarasi hiyo ilitolewa siku ya Jumapili ambayo sio siku rasmi ya kazi.

Kakulubelwa Mulalelo, katibu wa kudumu katika wizara hiyo aliambia kamati kwamba hana ufahamu ni nani aliruhusu kutolewa kwa kandarasi hiyo, na kwamba yeye alihudhuria uzinduzi na usambazaji wa bidhaa hizo pekee.

Raia wa Zambia waliopo katika twitter walitoa hisia zao kutokana na ufichuzi huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *