img

Marufuku kutoka nje Jamhuri ya Afrika ya Kati

January 8, 2021

Nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imetangaza ilani ya marufuku ya kutoka nje kutokana na sababu za kiusalama.

Waziri wa Mawasiliano na Msemaji wa Serikali nchini humo Albert Yaloke Mokpem, alitoa maelezo kwenye kituo cha redio ya taifa na kufahamisha kwamba Rais Faustin Archange Touadera ametangaza ilani ya marufuku ya kutoka nje kati ya saa 20.00 hadi 05.00.

Yaloke Mokpem aliongezea kusema kuwa uamuzi huo ulichukuliwa kwa lengo la tahadhari dhidi ya mashambulizi yanayoweza kutokea nchini humo.

Makundi ya waasi yaliyoko chini ya muungano wa chama cha CPC, yalitekeleza mashambulizi ya silaha hapo jana nyakati za asubuhi katika miji ya Buar na Grimari iliyoko upande wa Kusini Magharibi mwa nchi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *