img

Klabu Bingwa Afrika: Je Simba kuchomoka makundi na kutinga tena robo fainali?

January 8, 2021

Dakika 4 zilizopita

Simba imetinga hatua ya makundi baada ya kuifunga Platinum FC ya Zimbabwe 4-0 jijini Dar es Salaam.

Maelezo ya picha,

Simba imetinga hatua ya makundi baada ya kuifunga Platinum FC ya Zimbabwe 4-0 jijini Dar es Salaam.

Droo ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika imepangwa hii leo ambapo wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki Simba SC wamepangwa katika kundi la A Pamoja na mabingwa wa Afrika Al Ahly ya Misri.

Simba inashiriki hatua ya makundi msimu huu wa 2020/21 baada ya kushindwa katika msimu uliopita. Iliposhiriki hatua kama hiyo msimu wa 2018/19 ilikutana na Al-Ahly na Vita Club ya DRC ambao wapo kwenye kundi A tena msimu huu. Timu ya nne katika kundi hilo ni miamba ya Sudani El Merreikh.

Hivyo, ni sahihi kusema kuwa Simba, Al Ahly na Vita Club ni timu zinazofahamiana na zitakamiana tena msimu huu.

Walipokutana mara ya mwisho, Simba na Al Ahly ndiyo waliovuka kwenda hatua yar obo fainali.

Simba wamekuwa na rekodi nzuri nyumbani, katika msimu wa 2018/19 walifungwa goli 5 na Ahly na Vita walipokuwa ugenini, lakini Simba ilizifunga timu zote hizo jijini Dar Es Salaam.

Katika hali yoyote ile, kundi hilo ni gumu na klabu zote zitatakiwa kupambana kwa hali na mali kufuzu.

Simba inasifika kwa kuwa wakali nyumbani, na toka msimu wa 2018/2019 haijawahi kufungwa nyumbani katika michuano hiyo. Alama zote 9 walizopata msimu wa 2018/19 na kufuzu kwenda robo fainali walizipata katika uga wa Mkapa.

Kutokana na rekodi hiyo ya Simba, ni dhahiri kuwa timu zote zitajikaza na kupambana zaidi watakapocheza jijini Dar Es Salaam

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *