img

Kiongozi wa kidini anaehusishwa na shambulio la Bali aachiliwa

January 8, 2021

Kiongozi wa kidini mwenye itikadi kali anayehusishwa na shambulio la bomu kwenye kilabu moja ya burudani katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia ameachiliwa huru. 

Hatua hiyo imezua hasira miongoni mwa waathiriwa, ikiwa ni karibu miongo miwili imepita tangu kutokea shambulio hilo. 

Watu 200 wengi wao wakiwa watalii wa kigeni, waliuawa katika shambulio baya zaidi la kigaidi nchini Indonesia. 

Abu Bakar Bashir, 82, anatajwa kuwa ni kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Jemaah Islamiyah (JI) unaoongozwa kwa itikadi kali za Kiislam. 

Bashir alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mnamo mwaka 2011. Lakini hukumu hiyo ilifutwa baada ya kukata rufaa.

 Amekana kuhusika na shambulio hilo la bomu na bado haijulikani hasa alihusika kwa namna gani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *