img

Kaze atwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi

January 8, 2021

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/21.

Kaze ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba ambaye amebwaga manyanga na Francis Baraza wa Biashara United.

Yanga chini ya Kaze kwa mwezi huo ilishinda michezo minne na kutoka sare mmoja ikivuna pointi 13 na kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Yanga ilizifunga Ruvu Shooting FC (2-1), Mwadui FC (0-5), Dodoma Jiji FC (3-1) na Ihefu SC 0-3 huku wakitoka sare na Tanzania Prisons FC 1-1.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *