img

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya ziara nchini Uingereza kwa njia ya mtandao

January 8, 2021

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atafanya ziara mjini London kuanzia siku ya Jumapili. 

Kwa mujibu wa msemaji wake, Stephane Dujarric, ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hapo awali ilipangwa azuru Uingereza binafsi, lakini kwa sababu nchi hiyo imekumbwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona hilo halitawezekana na badala yake mikutano itafanyika kwa njia ya mtandao. 

Shughuli zake zitajumuisha hafla ya kuadhimisha miaka 75 ya kikao cha kwanza cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa, katika ukumbi wa Westminster mjini London. 

Mnamo Jumatatu na Jumanne wiki ijayo, Guterres atashiriki katika kikao juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na kisha atakutana kwa mazungumzo ya pande mbili na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, waziri wake wa mambo ya nje Dominic Raab na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby.

 Kulingana na msemaji wake Stephane Dujarric. Guterres anatarajiwa kutoa wito wa ushirikiano mpya ulimwenguni wa kuzishughulikia changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *