img

Elon Musk: Mimiliki wa kampuni ya Tesla atangazwa kuwa mwenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 185

January 8, 2021

Dakika 8 zilizopita

Elom Musk

Elon Musk amekuwa tajiri wa kwanza duniani huku thamani yake ikipita dola bilioni 185.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Tesla na SpaceX amechukua nafasi ya kwanza baada ya hisa zake za kampuni ya Tesla kuongezeka Alhamisi.

Amechukuwa nafasi ya kwanza na kumpiku mwasisi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos ambaye amekuwa akiorodheshwa wa kwanza kwa utajiri tangu mwaka 2017.

Thamani ya Bwana Musk mmiliki wa kampuni ya magari yanayotumia umeme ya Tesla imeongezeka mwaka huu na Jumatano ilifika dola bilioni 700 kwa mara ya kwanza.

Hatua hiyo inafanya kampuni yake ya magari anayomiliki thamani yake kuwa ya juu hata kushinda kampuni za Toyota, Volkswagen, Hyundai, GM na Ford kwa pamoja.

Bwana Musk alisherehekea taarifa hizo kwa aina yake, akimjibu mtumiaji mmoja wa Twitter aliyekuwa ameshirikisha wengine taarifa hizo kwa kuandika “inashangaza sana”.

Ujumbe wa twitter

Ujumbe wa awali uliokuwa juu ya ule wake uliangazia maoni juu ya utajiri wake.

“Karibu nusu ya pesa zake zimepangiwa kutatua matatizo ya dunia, na nusu yake zitasaidia kuwa na mji wenye kujitosheleza katika sayari ya mihiri yaani Mars, kuhakikisha uendelezaji wa maisha kwa spishi zote pengine ikifika wakati dunia idondokewe na kimondo kama vile dinosauri au kutokee Vita vya Tatu vya Dunia na pengine tujimaliza,” taarifa yake imesema.

Utajiri wa Musk umeongezeka kwasababu ya siasa za Marekani ambapo Democrats itakuwa na udhibiti wa bunge la Seneti katika kikao kijacho.

Daniel Ives, mchambuzi wa kampuni ya soko la hisa la Wedbush aliandika: “Kikosi cha Seneti cha Democratic ni imara na chenye uwezo wa kuleta mabadiliko kwa Tesla na sekta nzima ya magari yanayotumia umeme kwa ujumla, kukiwa na uhakika wa kuangazia zaidi ajenda za upunguzaji wa hatari ya mazingira katika kipindi cha miaka michahe ijayo.”

Bezos pia anatumia utajiri wake kufadhili safari za anga za mbali

Maelezo ya picha,

Bezos pia anatumia utajiri wake kufadhili safari za anga za mbali

Utajiri wa Bwana Bezos pia umekuwa ukiongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Janga la corona limefaidi kampuni ya Amazon kwasababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya manunuzi ya mtandaoni na huduma za kukusanya na kutunza data.

Hata hivyo, alitoa asilimia 4 ya mapato ya biashara zake na kumpa aliyekuwa mke wake ambaye wametengana MacKenzie Scott hatua iliyomsaidia Musk kumpiku.

Pia uwepo wa tishio la udhibti ni sawa na kusema kumechangia hisa za Amazon kutoongezeka sana kama ambavyo ingetarajiwa.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *