img

Dodoma yachukua Ubingwa Ligi Kuu Netiboli

January 8, 2021

Na John Walter-Manyara

Timu kutoka Dodoma imefanikiwa kuchukua taji la Ubingwa wa ligi kuu ya Netiboli mwaka 2021 baada ya kuifunga 45-44 Mjini Magharibi katika fainaloi iliyopigwa uwanja wa Kwaraa Mjini Babati mkoa wa Manyara.

Mashindano hayo yaliyoanza Januari 3 mwaka huu katika mkoa wa Manyara yamehitimishwa leo na mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti ambaye amesema ni heshima kubwa kuwa wenyeji wa  mashindano hayo kwani imesaidia kuutangaza mkoa na vivutio vyake.

Naibu Katibu Mkuu wa CHANETA Hilda Mwakatobe amesema mjini Magharibi kutoka Zanzibar ilikuja kama mwalikwa kwa lengo la kuendelea kudumisha Muungano ulioasisiwa na Viongozi wa nchi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Musa Misaile amesema michezo hiyo imekuwa fursa kwa wafanyabiashara wa mjini Babati kwa kuwa wameuza bidhaa mbalimbali katika kipindi chote cha Mashindano hayo.

Nafasi ya Pili imeenda Mjini Magharibi na  Mshindi wa Tatu imechukuliwa na timu kutoka mkoa wa  Arusha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *