img

COSITA yatoa Elimu kwa wajasiriamali Wanawake Babati

January 8, 2021

 


Na John Walter-Babati, Manyara

Katika kuhakikisha Wanawake wajasiriamali  wanafanya kazi zao kwa tija, Shirika lisilo la kiserikali COSITA limewapatia elimu kwa Wanawake zaidi ya 100 kutoka Mitaa 10 ya Halmashauri ya Mji wa Babati.

Baada ya semina hiyo, Wanawake wanaojishugulisha na usindikaji wa matunda na nafaka, wameomba  kupatiwa mikopo itakayowawezesha kuendeleza viwanda vidogo vidogo wanavyovimiliki ili kuboresha bidhaa zao na kukuza uchumi wao.

Mdau wa maendeleo mkoani Manyara Mkurugenzi wa shirika la COSITA lenye makao makuu mtaa wa Mruki  mjini Babati Patrice Gwasma, amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali juu ya kuzalisha bidhaa zenye ubora ili ziweze kupata masoko ya uhakika.

Amesema wanawafundisha wanawake wenye biashara ili wapanue biashara kupata elimu ya ujasiriamali na wasio na biashara waanzishe.

Kwa upande wake meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)  mkoa wa Manyara Abel Mapunda, amewataka wasindikaji hao kuchangamkia fursa za mikopo ya viwanda vidogo vidogo wanayoitoa.

Amesema mikopo wanayoitoa inasaidia sekta zalishaji  katika kuongeza mnyororo wa thamani kuanzia kwenye kilimo mpaka hatua ya mwisho 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *