img

Afisa wa polisi auawa akiwa hospitalini

January 8, 2021

Afisa wa polisi aliyejeruhiwa katika ghasia za uvamizi wa bunge la Marekani amefariki dunia. Hayo ni kwa mujibu wa idara ya polisi inayohusika na kulinda bunge hilo la Marekani. 

Afisa huyo wa polisi alifariki akiwa hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya katika ghasia hizo. 

Fujo hizo zilizofanywa Jumatano pia zimesababisha vifo vya watu wapatao watano. Mwanamke mmoja aliuawa baada ya kupigwa risasi na afisa wa polisi.

 Na mwananmke mwengine mmoja na wanaume wawili pia wameuawa kutokana na matatizo ya kiafya ambayo hayakufafanuliwa na polisi. 

Wabunge wawili wa chama cha Democratic wamesema waliohusika na ghasia hizo lazima wawajibishwe kwa vifo visivyoeleweka.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *